GET /api/v0.1/hansard/entries/1262896/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1262896,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262896/?format=api",
    "text_counter": 45,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ya kuwakaribisha waalimu wenzangu ambao wameongoza kikosi cha mabinti wenye nishati mpwito mpwito. Wamezuru Seneti siku ya leo kujionea kwa macho yale yanayoajiri hapa. Shule hii imo miongoni mwa shule zinazobobea kimasomo katika Kaunti ya Bungoma. Ni shule mojawapo ambayo kiongozi wa akina mama Mhe. Catherine Wambilianga alizindua mchakato wa kuboresha masomo na fedha za bursary katika Kaunti ya Bungoma. Ni shule mojawapo ambayo waasisi wake ni kanisa la Friends . Shule hii inatambulika kwa michezo, uimbaji wa kwaya na talanta mbalimbali. Mimi ninajivunia waalimu na wanafunzi ambao wako hapa. Ni kielelezo kwamba Bungoma ina uwezo wa kimasomo na talanta ambazo kwa muda mrefu zimepuuzwa na wengi nchini. Nina furaha kwamba wamefika hapa kujionea mwalimu Wafula akiboronga na kukinyorosha Kiswahili, akiwasilisha hoja za Bungoma na nchi nzima mchana peupe pasipo kutishwa ama kutikiswa na mtu yeyote. Hii ni shule ya wasichana na ningependa mjionee. Kuna Maseneta akina mama ambao hutetea hadhi na nafasi ya wanawake nchini Kenya. Sio kwa sababu ni wanawake lakini wamepigiwa kura na kuteuliwa na vyama vya kisiasa ambavyo zinaamini katika demokrasia na nafasi ya akina mama kama uti wa mgongo wa nchi ya Kenya. Leo mmejionea na mmeshika kovu kama Tomaso kwamba japo nyinyi ni wasichana, muna nafasi ile ile kama vijana barubaru katika Kaunti ya Bungoma kupata nafasi na mgao wenu nchini. Sisi Serikali ya Kenya Kwanza tutawatetea wasichana na wavulana ili katika mgao na rasilimali za nchi ya Kenya, wote waweze kunufaika sio kwa sababu ya jinsia ila uwezo wako wa kusoma na kuandika, na kupambana na changamoto za kiuchumi. Bw. Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii. Ningependa uwape nafasi kupitia mamlaka yako, wanywe chai na wajivijari katika Bunge la Seneti."
}