GET /api/v0.1/hansard/entries/1262910/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1262910,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262910/?format=api",
"text_counter": 59,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza, nataka kumpa kongole aliyeleta hii Petition ndani ya Bunge hili la Seneti, kuomba ya kwamba, Bunge la Seneti litaweza kuingilia kati kuona kuwa wale wakulima wanaolima mahindi katika maeneo ya Bomet na Nandi wanaoongozwa na ndugu yangu Sen. Cherarkey wamepata afueni na misaada inayohitajika ili kuona kwamba mazao ya mahindi kule yamefaidika. Bw. Spika, Ardhilhali hii sio ya watu wa Kaunti ya Bomet pekee yake bali Kenya nzima, hata Kaunti ya Kilifi. Sote tunategemea kilimo cha mahindi ili tupate faida wakati wa mavuno. Mavuno haya yatatukinga kutokana na njaa, kuwapa wananchi afya na vile vile pesa iwapo watauza hayo mahindi."
}