GET /api/v0.1/hansard/entries/1263046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1263046,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1263046/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Nafikiri ni kwa sababu ya likizo. Kumekuwa na msemo kwamba wengi wetu huwa hatukuji Bungeni. Ni jambo la kusikitisha sana. Kwanza, watu huja Bungeni kukiwa na Mswada ama mtu ameambiwa aje kwa sababu ya kitu fulani. Mienendo kama hiyo haitatusaidia. Wewe ulichaguliwa na wananchi uje kwenye Seneti, utunge sheria ambazo zitasaidia na kutetea kaunti uliochaguliwa. Lakini, ni jambo la kusikitisha kuona hususan watu ambao walichaguliwa ndio hawaji kwenye Bunge. Sen. Thang’wa amesema kwamba ingekuwa vizuri tuwe na kamukunji ili tuulizane maswali kwa kina na kwa uwazi, ili tujue kwa sababu gani watu hawataki kuja Bungeni? Kiongozi wa walio Wengi atakubaliana na mimi kwamba Bunge lilikuwa likijaa sana miaka ya 2013, 2014, 2015 na hata Bunge lililopita. Bw. Spika, tunakaribia mwisho wa mwaka tangu tuanze hili Bunge. Ninasikitika ya kwamba wakati mwingine unapoingia ndani, ndio kengele inapigwa. Hiyo sio kawaida. Kawaida ya Bunge ni sisi sote tuingie hapa ndani na tukae, halafu wewe ukiingia baadaye, utakuta Bunge limejaa. Sio kuitwa na kengele. Ninawauliza hawa ndugu zangu, Viranja wa Upinzani na wa Walio Wengi Bungeni, wanastahili kujua na kufanya kazi yao vizuri. Ninawapatia kongole kwa sababu wanafanya kazi. Hata huu upande wetu, wanafanya kazi. Lakini sasa itabidi tuite"
}