GET /api/v0.1/hansard/entries/1263124/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1263124,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1263124/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda kwa fursa hii ambayo umenitunuku ili nikaribishe wanafunzi na walimu wa Friends School, Bwake. Chanzo cha jina Bwake ni Kaunti ya Bungoma. Hii ni ishara kwamba kitaasisi ama kiafrika, watu hugura kutoka eneo moja hadi lingine. Hawa jinsi walivyo hapa, ni ndugu zangu kutoka Kaunti ya Trans Nzoia. Wazazi wao walitia jitihada ili wawe katika uhai huu na shule hii. Walimu vilevile ambao wamehakikisha wanafunzi wamekuja hapa, wanaelewa kwamba, jukumu la Bunge la Seneti ni kutunga sheria. Hususan, kudhibiti matumizi ya fedha katika kaunti, kutunga sheria, kuafiki malengo ya ugatuzi na pia kupambana na ufisadi katika kaunti. Langu ni kuwakaribisha wanafunzi kutoka Kaunti ya Trans Nzoia. Nyinyi na Kaunti ya Bungoma ni kama mapacha ambao wanafanana kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ninawahakikishia kwamba changamoto ambazo huwapata nyinyi watu wa Kaunti ya Trans Nzoia, huwafikia watu wa Kaunti ya Bungoma. Pamoja na Seneta wenu, ndugu yangu, Sen. Chesang, tutahakikisha kwamba miundo mbinu, idadi ya walimu katika shule na mazingira mufti ya wanafunzi na walimu kufanya kazi yatadumishwa ili kuhakikisha kwamba mnapata yale mnataraji katika shule; na wazazi vilevile wanufaike katika matokeo ambayo mtapata. Sisi kama Serikali, tutahakikisha kwamba fedha zinakuja wakati unaostahili na kwamba pia mnanufaika na kufurahia. Bi Spika wa Muda, ndugu yangu, Seneta wenu, amewasili. Ningependa yeye kama pacha wangu wa Kaunti ya Bungoma, nimkaribishe kupitia kwa idhini yako, akaribishe vijana chipukizi kutoka Kaunti ya Trans Nzoia. Ni vizuri wasikie sauti yake na wapate mawaidha na baraka zake. Baadaye, atawapa ya Kaisari baada ya kuhudumia Buynge la Seneti."
}