GET /api/v0.1/hansard/entries/1263144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1263144,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1263144/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bi. Spika. Naunga mkono Kamati inayoenda kuangalia vile watu waliumia. Ni ajabu kwamba kumekuwa na ajali kwa miaka mingi. Utakuta kuna zingine kuna insurance, na zingine watu wakienda kotini wanalipwa. Unakuta kwamba gari likianguka, mtu analipwa kwa kipindi cha miaka miwili au mitatu. Ni jambo la aibu sana kwamba kuna watu waliumia na wakafa, wengine walipoteza wazazi ambao walikuwa na watoto na mabibi ambao walikuwa wanawategemea, lakini mpaka leo; miaka 25 iliyopita, wale watu waliwachwa na sasa wamekua masikini hata hawawezi kusomesha watoto wao wala kufanya jambo lolote. Wengine waliumia na familia zao zikasambaratika. Wengine wanatembea na magari kwa sababu mikono yao ama miguu yao ilikatwa. Wengine walikuwa wanafunza lakini saa hii hawawezi kufanya kazi yoyote. Wengine wako hali mahututi na wengine waliaga dunia. Saa hii ni miaka ishirini na tano. Kwa hivyo ninaunga mkono kwamba nchi ya Marekani iweze kuangalia vile hawa watu wataweza kulipwa pesa zao. Ni aibu kwamba jambo kama hilo lilifanyika na lilikuwa linahusu Wamarekani ambao wanajivunia kwamba, wako na pesa na hawajalipa watu wetu wa Kenya. Naunga mkono."
}