GET /api/v0.1/hansard/entries/1263223/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1263223,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1263223/?format=api",
    "text_counter": 372,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda. Nimesimama hapa siku ya leo kuunga mkono Hoja hii ambao umeletwa na Sen. Kavindu Muthama kwa sababu janga lilotukumba mwaka 1998 ni janga ambalo kila Mkenya anasikia uchungu. Mnamo tarehe 7 Agosti, 1998, Mohammed Rashed alifikishwa kortini kule Marekani na akashtakiwa kwa kuwaumiza watu 12. Hao watu 12 walikuwa wananchi wa America ambao walikuwa wameumia. Hawakutaja kwamba Wakenya 224 walikuwa pia wameumia. Waliohukumiwa baaadaye ndio walikuja sasa kubadilisha ile nambari ya watu waliokuwa wameumia. Mnamo tarehe 5 Agosti 2020, America ilisema kwamba kuna pesa ya ridhaa ambayo ilikuwa inafaa kulipwa watu walioumia ambayo ilikuwa takriban US$10.2 bilioni. Mnamo tarehe 31 Machi, 2021, aliyekuwa Secretary of State, Antony Blinken, alipokea kitita cha USD335 milioni kutoka nchi ya Sudan, ambayo ilikuwa imepatikana na makosa ya kuwaficha magaidi ambao walishambulia Kenya mwaka wa 1998. Walikuja na Omnibus Bill ambayo ilisema kwamba watu ambao wangefidiwa ni raia wa Marekani pekee. Endapo uliumia na hukuwa raia na ukaenda Marekani, basi ungepewa pesa kidogo kushinda waliokuwa kule. Huwa najiuliza swali. Hakuna uhai mkubwa kushinda mwingine. Wakati pesa ilipokuwa inagawanywa, ilifaa kuangalia maslahi ya Wakenya walioumia katika mlipuko wa huo wa bomu. Wakenya waliumia kwa sababu walikuwa wamehifadhi raia wa Marekani katika jumba hilo. Hiyo ndio sababu magaidi hawakuenda katika KICC ama Central Bank ofKenya (CBK) . Walienda moja kwa moja katika jumba lile. Naunga mkono kuundwa kwa Kamati hii. Wanakamati wana jukumu la kuhakikisha kwamba walioumia wanapata haki. Si haki peke yake bali pia fidia kwa sababu wameteseka kwa muda mrefu."
}