GET /api/v0.1/hansard/entries/1263846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1263846,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1263846/?format=api",
    "text_counter": 607,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": ". Kama alivyosema Mheshimiwa mwanzangu hapa, kuna utata katika anga zetu za bahari. Ni vizuri kujua mahali mipaka ya jirani wetu Somalia imefika ili wasituingilie. Itakua vizuri sana kukinga anga zetu za bahari ili tuvune pakubwa. Nilikuwa na wivu sana nilipoona boat zimepelekwa katika Kaunti jirani ya Kwale. Naambia Serikali kwamba wananchi wa Mombasa wanalia. Ikiwa walipeleka fishing boats kule Kwale, tunaomba hata sisi wavuvi wetu wanaotumia boats ndogo ndogo ama ngarawa ndogo ndogo kwenda kuvua samaki pia wapewe speedboats . Hata ikiwezekana, Serikali iwatengenezee meli kubwa ya kuvua samaki. Licha ya hayo yote, naunga Mjadala huu mkono. Bahari ni muhimu; bahari ni maisha na maji ni maisha. Hata ikiwezekana, tunaweza tukatoa maji ya bahari tukayasafisha ili yatumike katika majumba yetu ili watu wapate maji safi. Kwa hivyo, muhimu ya yote ni kuwa naunga mkono Mjadala huu. Tukinge anga zetu za bahari na si bahari ya Mombasa peke yake, hata pia Ziwa Victoria pia iangaliwe na magugu yaliyomo yatolewe ili wavuvi waweze kuvua samaki. Tukifanya hivyo, tutakuwa na chakula cha kutosha hapa Kenya. Wavuvi na wananchi watafurahi. Uchumi utainuka na uchumi wa samawati utasherekewa kila sehemu ya Kenya. Bandari inategemea bahari. Bila bahari kuwa sawa, hata yale mazao ambayo yanatoka bandarini hayatakuwa mazuri. Ikiwa hakuna ulinzi wa kutosha pale ndani ya bahari, pia wale The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}