GET /api/v0.1/hansard/entries/1264286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1264286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1264286/?format=api",
"text_counter": 383,
"type": "speech",
"speaker_name": "Butere, ODM",
"speaker_title": "Hon Nicholas Mwale",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Pia nami ningependa kuchangia hii Hoja ya ukosefu wa usalama katika Kaunti ya Lamu. Wakati ambapo hamna usalama katika eneo lolote nchini, ni akina mama, watoto na vijana ambao wanateseka zaidi. Wacha nianze kwa kumshukuru mwenzangu, Mbunge wa Eneo Bunge la Lamu kwa kuileta Hoja hii kuhusu utovu wa usalama katika Kaunti yetu ya Lamu. Usalama haujakosekana kule Lamu peke yaka bali pia katika maeneo mengine humu nchini. Kwenye maeneo mengi humu nchini, watu wanateseka, wengine wanapoteza maisha na wengine kunajisiwa."
}