GET /api/v0.1/hansard/entries/1264292/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1264292,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1264292/?format=api",
    "text_counter": 389,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Butere, ODM",
    "speaker_title": "Hon Nicholas Mwale",
    "speaker": null,
    "content": "Naibu Spika wa Muda, ili uchumi wetu uweze kukua, ni lazima tuimarishe usalama. Pasipo na usalama wanafunzi hawawezi kwenda shuleni, na wafanyibiashara pia hawawezi kufanya biashara. Mambo mengi yanazungukwa na usalama. Kwa hivyo ni lazima Serikali idumishe usalama. Kuna vifaa kwenye vikosi vya polisi na jeshi vilivyonunuliwa kutumia ushuru kutoka kwa wananchi. Vinafaa hivyo vitolewe vipelekwe Lamu na mahali kwingine inchini kwenye utovu wa usalama. Hivyo vifaa vinafaa vitumike kuwalinda wananchi ambao wanalipa ushuru. Tuko na wanajeshi ambao wamepelekwa nchini Congo kudumisha amani. Hivi majuzi, vyombo vya habari vilitangaza kwamba Serikali ya Congo inayoongozwa na Rais Felix Tshisekedi haiwataki wanajeshi wetu nchini kwao. Mbona tusiwarudishe na tuwapeleke Lamu ile wawalinde Wakenya? Ninaunga mkono Hoja hii ili usalama udumishwe katika Kaunti ya Lamu na kwingineko nchini Kenya ndiyo wananchi waweze kuishi wakijua kwamba tuko na wanajeshi na askari wa polisi ambao wanawalinda . Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}