GET /api/v0.1/hansard/entries/1264961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1264961,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1264961/?format=api",
    "text_counter": 605,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "ndani ya bahari, ni Mchina aliyeingia na meli yake. Yeye huvua samaki kisha anatuuzia kwa bei ghali. Ningependa kuambia Serikali idhibiti maeneo yetu ya bahari ili wavuvi wetu waingie baharini, wavue samaki na wawauze hapa nchini ili uchumi wetu uinuke. Tunaweza kufanya wenyewe packaging ya samaki wanaovuliwa baharini na tupeleke mataifa ya ng’ambo. Ukingo wa bahari una mambo mengi ambayo yanaweza kuwasaidia wananchi wanaoishi katika kingo za bahari, haswa Mombasa. Tukiweza kutenga sehemu ambazo, kwa mfano, watu kama wale wa Kamba craft watatengezea vitu vyao vya kitamaduni na kuviuza, itakuwa bora kwa sababu sehemu hizo huvutia watalii. Watalii wakija na wapate mambo mazuri yamezunguka kingo za bahari yetu, Kenya itazidi kuwa na uchumi mzuri kutokana na utalii. Vile vile, wawekezaji wadogo kama Kamba craft, wasanii wafanyao sanaa kando kando mwa bahari na wauza nguo za kuswim watapata mazao mazuri. Kwa hivyo, tulinde bahari zetu na anga za bahari zetu. Tuhakikishe pollution haiingii ndani ya maji. Meli zipitapo, zingine humwaga mafuta baharini na samaki hufa. Kuna sehemu ambazo huelekeza maji taka ndani ya bahari. Hili ni Jambo ambalo huleta madhara mengi kwa wananchi na kwa ecosystem ya viumbe vya baharini. Jambo hili linatendeka hata Mombasa. Sehemu kama Tudor, maji taka huelekezwa ndani ya bahari na watoto wanaogelea pale. Tukiweza kukinga bahari yetu na kumiliki anga za bahari yetu, tutaboresha uchumi wa samawati yaani blue economy na Kenya itavuna mazao makubwa. Tunapoangazia uchumi samawati, hatuangalii tu kingo za bahari yetu peke yake. Tuwaangalie wawekezaji ambao wanatumia bahari kuja kwetu na tumiliki anga zetu vizuri ili wasikutane na"
}