GET /api/v0.1/hansard/entries/1265051/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1265051,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1265051/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
"speaker": null,
"content": " Asante Naibu Spika. Naunga mkono kaka yangu Mhe. Bady Twalib, anayejiita Fula Ngenge . Ninaungana naye kuomba Serikali na hasa Tume ya Taifa ya Ardhi wafidie watu wa Jomvu. Makadirio ya malipo yalifanywa na pesa ziko, lakini wafanyakazi wengine na wakubwa wengine ambao wameongeza mambo ambayo hayamo wamesababisha watu wa Jomvu kukosa kulipwa fidia. Ninajua kuna ujanja pale. Wanataka kuwanyaganya riba ya hizo pesa zote ambazo zilikuwa ni za kufidia wananchi wa Jomvu. Wakaazi wa Jomvu ni Wakenya sawasawa na Wakenya wengine ambao walifurushwa makao yao. Kwanza barabara ya Madafuni ni mbaya sana. Wakaazi wa Jomvu walitolewa kwa nguvu bila kulipwa fidia. Majangili ambao wanakataza haki ya watu wa Jomvu wakabiliwe na watu wa Jomvu wapate haki yao. Ninamuunga mkono Mhe. Bady Twalib. Asante."
}