GET /api/v0.1/hansard/entries/1265357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1265357,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1265357/?format=api",
    "text_counter": 337,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Nimesimama kuunga mkono Ripoti hii. Taifa bora ni lile linalolinda mazingira yake. Mazingira ndio chanzo cha matatizo mengi. Mataifa mengi yanarudi nyuma wakati mazingira yanakuwa mabaya. Mazingira yanapokuwa mabaya, maradhi yanagubika taifa hilo. Na badala ya kwenda mbele, linarudi nyuma. Siyo vyema watu katika mataifa mengine ambayo ni ya kitajiri kutupa takataka zao sehemu zetu. Au hata mabaki ambayo wanaona hayawafai na kusema sasa yanakuja kama msaada na kumbe yana madhara."
}