GET /api/v0.1/hansard/entries/1265358/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1265358,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1265358/?format=api",
    "text_counter": 338,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Bahari yetu imechafuliwa sana na mataifa yanayojiita ya kitajiri. Licha ya kuwa tuna umaskini, hao ndio wametusababishia umaskini huo kwa njia kama hii ya kutuletea uchafu ambao ni sumu. Tabia hiyo yao inaturudisha nyuma na wao wanatuambia kuwa wanakuja kutupa misaada. Maradhi ya saratani hayakuwa hapa Afrika hapo zamani. Sasa yamezidi mpaka mtoto mdogo anazaliwa na hayo maradhi kwa sababu ya ule uchafu wanaotubwagia. Kule kwao, wanajifanya wanasafisha bahari zao, lakini kwetu ndio wanatumia kama dumping grounds na kusema ni msaada. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}