GET /api/v0.1/hansard/entries/1265359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1265359,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1265359/?format=api",
    "text_counter": 339,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Taifa linaloheshimika ni lile ambalo linahakikisha kwamba watu wake wanaishi salama. Kuishi salama ni kutokubali kabisa kumwagiwa vitu usivyovijua. Wanatuletea vifaa, kama wanavyosema, vinakuja kama msaada lakini baada ya wiki mbili vinaharibika na tayari vilishatoa miale fulani kwa wale watoto kama ni vya shule. Ni vyema twende na hali yetu wenyewe. Tusijaribu kuomba misaada ambayo itakuja kutudhuru. Hata sisi katika taifa letu, ikiwa ni takataka ambazo ziko katika sehemu ya mji mwingine, zisihamishwe kupelekwa mji mwingine. Zikae pale pale na kama zina madhara, basi zikabiliwe pale na zisiambukize sehemu nyingine."
}