GET /api/v0.1/hansard/entries/1265369/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1265369,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1265369/?format=api",
"text_counter": 349,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "Mara kwa mara, tumekuwa tukiona mambo ambayo wakati mwingine hayapendezi kwa sababu licha ya kwamba pengine tunatumiwa takataka, kuna wakati ulifika tukaja tukaambiwa sukari inayoletwa humu nchini ina madhara. Lakini, kwa sababu ya tamaa ya kutaka kujitajirisha mapema, watu fulani humu nchini wakaamua kwamba maisha ya binadamu si muhimu, bali utajiri ambao wanautafuta. Mambo haya yamekuwa yakiendelea na vitengo vinavyohusika viko lakini hatua haichukuliwi. Unakuta mambo yale yanapotea kwa upepo. Hatuna roho mbadala kwamba pengine baada ya kupata shida kama zile, tunaweza tukaenda tukaomba roho nyingine ili tuwapatie watu wetu. Tunapopewa maradhi, tunahangaika na kutafuta kitu kitakachoweza kutuokoa."
}