GET /api/v0.1/hansard/entries/1265370/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1265370,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1265370/?format=api",
"text_counter": 350,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "Kamati hii imefanya kazi ya kutosha na letu ni kuwapa pongezi kwamba kazi walioifanya ionekane na mwangaza huko mbele. Likiwa ni funzo kwamba Bunge hili linapitisha Hoja hii, basi inatakikana kwamba baada ya hii, sheria mwafaka ikafuate ili tupate kuhakikisha kwamba tunafunga milango yote inayoweza kutumiwa na wale ambao wanaona Kenya kama mahali pa kufanya lolote lile kimajaribio. Sisi si raia ambao pengine hatuna umuhimu kwa Mwenyezi Mungu. Huu umaskini ambao tuko nao sio kwamba tulitaka tuwe hivi. Watu wasichukulie umaskini huu kuwa unyonge na kuwa wanaweza kutufanyia mambo vile wanavyotaka. Naipongeza Kamati, na nalipongeza Bunge hili kwa sababu ya kuiunga mkono Hoja hii ili kuhakikisha kwamba tunatafuta usalama kwa wananchi wetu. Miaka miwili au mitatu iliyopita, tulikuwa na maradhi ya Corona. Maradhi hayo, tukiyaulizia zaidi, tunapata yalitokana na baadhi ya watu fulani kueneze ugonjwa huo kwa sababu walikuwa wanafanyia madawa yao majaribio. Mataifa yamewahi kufanya majaribio ya silaha zao hatari katika Bahari Hindi. Kule kuna samaki tunaowatumia. Mwisho tunapatikana na matatizo ya maradhi. Mambo haya yote yanatuumiza sisi wananchi. Kwa hivyo, naomba sheria ipitishwe ya kuhakikisha kwamba tumefunga njia zote za wahalifu wanaotumia nafasi kama hii kutuletea vitu ambavyo vinaweza kutuletea madhara. Nakushukuru Mhe. Spika wa Muda kwa sababu ya kunipa nafasi. Ninakotoka ni mahali ambapo najua mambo haya yapo. Kwa sababu ya ukosefu wa elimu, watu wengi hujiingiza mashakani. Kwa hivyo, naiunga mkono na nasema Mungu atubariki kwa hayo. Ahsante."
}