GET /api/v0.1/hansard/entries/1267253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1267253,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267253/?format=api",
"text_counter": 446,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie yale ambayo Sen. Maanzao ametaja. Katiba inatupa ruhusa ya kumiliki mali na rasilmali hapa Kenya. Yale yanayojiri ni kinaya na kinyume na matarajio ya wanademokrasia hapa Kenya. Sisi Wakristo tunajua kuwa maandamano ni kubeba matawi na mabango kwa amani. Tumekuwa tukishuhudia maandamano ya madaktari, walimu na wakulima. Wakati wa maandamano, hatujawahi kuwa na bughdha au purukushani yeyote, uharibifu wa mali na watu kuumia. Sijui wanademokrasia hao wanaandamana kushinikiza nini. Sijui wanataka tupoteze maisha ya watu wangapi ili wajue kuwa ni maandamano. Sijui wanataka watu wangapi wajeruhiwe ili waseme kuwa ni maandamano. Wakenya walipokuwa wanalima mashamba, walikuwa wanabeba sufuria wakitembea. Wakenya walipoenda kuchukua mbolea katika maghala ya halmashauri ya nafaka, watu hao walikuwa wanabwata na kutembea. Wakenya walipokuwa wanapuliza"
}