GET /api/v0.1/hansard/entries/1267255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1267255,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267255/?format=api",
"text_counter": 448,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "dawa kwa mahindi, ndungu zangu walikuwa katika vyombo vya habari wakibwata. Sasa karibu watu wanavuna. Badala ya kuandaa sufuria kukaribisha mavuno ya kipekee, ndugu zetu wametoa vijana wenye misuli na uwezo wa kujenga nchi. Wanaenda kwenye baraste za nchi hii wakipiga mayowe na kubeba sufuria kwenye vichwa. Sijui ni dini gani, tamaduni au itikadi zipi zinazowaruhusu wasomi wa tajriba kama hawa katika Seneti kubeba sufuria kwenye vichwa kadamnasi ya vyombo vya habari dunia nzima. Ukiweka sufuria kwenye kichwa, sijui kama bei ya bidhaa na chakula itashuka. Sijui ni maombi gani wanayotarajia. Katiba inatupa nafasi ya kutembea na kuhusiana na watu mbalimbali. Sasa tunashuhudia kufungwa kwa barabara na magari kuteketezwa. Sijui Wakenya watakuwa wageni wa nani. Wakenya watapata huduma za usafiri, matibabu na usalama vipi iwapo maandamano ya kidemokrasia yanaweza kusababisha kuteketezwa kwa bidhaa katika miji ya Kenya. Sijui wanataka tuteketeze mali kiasi kipi ili wajue kwamba ni maandamano. Hii ni Seneti ya taifa la Kenya. Watu wawe huru kuja kujieleza na kujitetea. Kuna Bunge la kitaifa; watu waje wajitetee. Hivi sasa, tumekuwa tunatunga sheria mbali mbali za kilimo na ufugaji."
}