GET /api/v0.1/hansard/entries/1267386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1267386,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267386/?format=api",
    "text_counter": 579,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Maandamano ambayo inaendelea inaongozwa na wananchi wa Kenya ambao wanajitetea na kudai haki yao. Si kwamba maandamano imepangwa na viongozi wa Azimio kwa sababu, Wakenya wenyewe ndio wanaumia. Bi. Spika wa Muda, kutokana na yale mambo yanayoendelea, kusema kwamba Wakenya wanasukumwa kuenda kuuliwa ni uongo. Tunajua vizuri sana kwamba Katiba yetu ya Kenya inapea mwananchi nguvu na uwezo na na haki ya kuunga kutetea haki yao. Kwa hivyo, ile haki mwananchi ako nayo na ameipitisha kwa viongozi, anaweza dai hayo mamlaka na airudishe ndiposa adai haki yake. Hii ni Bunge ya heshima. Kwa hakika wanananchi wanatutegemea kama Seneti. Itakuwa ni vibaya sana kama kutasimama kiongozi hapa aseme uongo kwamba wale wanaenda maandamano ndio wanasabisha uharibifu wa mali na vifo. Tunajua vizuri sana kwamba sisi wana Azimio tungewachwa tuende kwa barabara kudai haki yetu bila kuingiliwa na polisi au wahuni ambao wanapangwa na maseneta kama Sen. Cherarkey, basi hakungekuwa na vurugu yoyote."
}