GET /api/v0.1/hansard/entries/1267456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1267456,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267456/?format=api",
    "text_counter": 649,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia hoja ambayo imeletwa Bungeni na Seneta wa Embu, Sen. Munyi Mundigi. Kwanza kabisa, ninampongeza Seneta wa Kaunti ya Embu kwa kuleta Hoja hii alasiri ya leo. Mapema, alikuwa ameomba taarifa hapa kwa nini watu wake wamekosa mbolea ili waweze kupanda miti na wazalishe chakula kwa uzuri zaidi kwao. Pia, nilisikia kwa masikitiko mchango ulioletwa na Sen. Wafula, Seneta wa gatuzi la Bungoma, ambaye anawakilisha chama cha Ford Kenya katika Bunge hili. Chama ambacho ndio baba na mama wa upinzani katika nchi yetu ya Kenya. Hayati Masinde Muliro, hayati Kijana Wamalwa, na wengineo ambao walipigania demokrasia katika nchi hii yetu leo wanageuka katika makaburi yao kwa sababu ya matamshi ambayo ametoa Mheshimiwa Wafula. Bi Spika, wa Muda, katiba ya Kenya inatupa fursa kuandamana. Inatupa fursa ya kugoma na kulalamika kwa mambo ambayo hayastahili kufanyiwa Wakenya. Mswada wa fedha uliopitishwa na Bunge mwezi uliopita ni Mswada ambao asilimia 90 ya Wakenya waliupinga. Lakini, Wabunge wachache katika Bunge lile 170, walipitisha ni sawa iwe sheria katika nchi yetu ya Kenya. Wale wengi ambao hawakupata fursa ya kuzungumza katika Bunge lile, wale wengi ambao maoni yao yalikataliwa katika vikao vya ushauri wa umma yaani; public participation ndio wale wananchi ambao sasa wako tayari kuandamana kupinga sheria hii. Imeelezwa hapa kwamba mkurupuko wa bei ni kwa sababu ya mambo ya Ukraine. Hiyo sio shida. Mukrupuko wa bei ni kwa sababu ya siasa duni na policy duni"
}