GET /api/v0.1/hansard/entries/1267467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1267467,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267467/?format=api",
"text_counter": 660,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi Spika wa Muda, sikusema kwamba ni Serikali ya Kenya Kwisha. Nimesema Kenya Kwisha. Kuna tofauti ya Serikali ya Kenya Kwisha na neno Kenya kwisha. Mungenisikiza kwa makini kwa sababu mnataka kulifanya Bunge la Seneti kuwa kama yale mabaraza ya mitaa kule mnakotoka. Madam Temporary Speaker, polisi ndio chanzo kikubwa cha kutawanya na kukurupuka kwa maandamano katika nchi yetu ya Kenya. Kulingana na takwimu na vile vile mambo ambayo yalinipata mimi mwenyewe binafsi kama Seneta wa Mombasa. Tarehe kumi na mbili, jumatano iliyopita, tulikuwa tumetoa arifa ya kuandamana katika Kaunti ya Mombasa. Taarifa ilipelekwa mapema kwa polisi lakini polisi walikaa hadi saa mbili asubuhi wakati tuko tayari kuandamana na wakaleta barua kusema kwamba maandamano ni marufuku kwa sababu ya utalii. Bi Spika wa Muda, ninachangia Hoja ya Sen. Munyi Mundigi na yeye ndiye wa kwanza kupiga kelele. Lazima wakati ujao tukija hapa Bunge, watu wapimwe wamekula miraa ama mogoka kiasi gani."
}