GET /api/v0.1/hansard/entries/1267472/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1267472,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267472/?format=api",
    "text_counter": 665,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi Spika wa Muda, wajua Sen. Cherarkey tulimlea sisi hapa. Hata mimi ndiye nilimsaidia mpaka akaapishwa kama wakili. Heshima ni kitu muhimu. Yeye amekuwa nje ya Bunge, ameingia tu na kuanza kuruka na kusema kwamba mambo ya miraa hivi na vile. Zingine huwa sio hoja za nidhamu; ni mtu apate tu fursa ya kupiga kelele. Hakuna chochote kilichokosa nidhamu hapo. Nimesema kwamba, kuwekwe mashine ya kupima watu kama wamekula miraa ama mogoka. Hiyo haimaanishi tumetusi mtu yeyote. Kwa kumalizia, ni kwamba polisi ndio watu wa kwanza kuvuruga maandamano."
}