GET /api/v0.1/hansard/entries/1267556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1267556,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267556/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono dua iliyoletwa na wafanyikazi wanaosimamia ugavi katika vituo vyetu vya afya. Ni ukweli Katiba yetu inasema dhahiri shahiri hakuna mtu anapaswa kubaguliwa. Wamesema vizuri katika ombi lao kwamba wanabaguliwa, ilhali wanahusika kwa mambo manufaa katika hospitali zetu. Wao ndio wanapokea na kuhifadhi. Vilevile, utapata wanasaidia katika ile hali ya kupeana dawa. Lakini, ikifika ni mambo ya kulipwa marupurupu yao, hawaangaliwi. Wanawekwa kando. Wanafanya kazi za dharura. Wakati mwingine, wanakuja kazini hata mwisho wa wiki wakati wafanyikazi wengine hawako. Kwa hivyo, wanafanya kazi ya muhimu. Lakini, ikiwa wao watabaguliwa katika gatuzi zetu, itakuwa ni jambo la kuvunja moyo sana. Naunga mkono ombi waliloleta. Liangaziwe kwa kindani na lishighulikiwe na Kamati ya Afya ambayo inaongozwa na Seneta ambaye amejitolea na tunajua anafanya kazi yake vizuri. Hawa ndugu zetu amabo wanafanya hii kazi ya kusimamaia ugavi waweze kuangaliwa na kupatiwa kilicho chao."
}