GET /api/v0.1/hansard/entries/1267616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1267616,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267616/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, naunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Nyamu. Katiba yetu inasema kuwa vijana, akina mama na watu wanaoishi na ulemavu wanafaa kupewa fursa ya kufanya biashara na serikali zetu. Kuna baadhi za kaunti zinazowapa makundi niliyotaja fursa ya kufanya biashara. La muhimu sio tu kupewa fursa ya kufanya biashara. Hata wanapopewa fursa ya kufanya biashara, utapata kuwa hawalipwi. Wanafaa kusaidiwa baada ya kuchukua mikopo kwenye benki. Hiyo haifanyiki tu katika kaunti zetu bali pia katika Serikali ya kitaifa. Kamati itakayoshughulikia Taarifa hii inafaa kuangazia zaidi mambo hayo. Vijana, watu wanaoishi na ulemavu na akina mama wanafaa kulipwa baada ya kupewa fursa ya kufanya biashara. La manufaa zaidi sio tu kufanya biashara bali kulipwa ili angalau wapate afueni katika hali yao ya maisha."
}