GET /api/v0.1/hansard/entries/1267618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1267618,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267618/?format=api",
    "text_counter": 100,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, naunga mkono Taarifa hii. Mambo ya AGPO yanafaa kuangaliwa vizuri kwa sababu kwa miaka mingi, vijana, akina mama na watu wanaoishi na ulemavu wamekuwa wakinyanyaswa. Utapata matajiri wengi wanasajili kampuni kutumia majina ya vijana, akina mama na watu wanaoishi na ulemavu. Uchunguzi unafaa kufanywa kujua wamiliki halisi wa kampuni ili kuhakikisha kuwa vijana, akina mama na watu wanaoishi na ulemavu wanapewa fursa ya kufanya biashara na serikali zetu. Magavana na viongozi wengine serikalini wamekuwa wakifaidika kutumia majina ya watu wengine. Kuna wakati nilikuwa napewa kandarasi--- Watoto wetu wanapoanzisha kampuni baada ya kumaliza shule, inakuwa shida kulipwa. Kwa hivyo, uchunguzi unafaa kufanywa kwa magavana na mafiasa wengine wakuu serikalini. Kama wanataka kusaidia vijana wetu, basi wawe wakiwalipa ili wafanye kazi inayofaa. Asante, Bw. Spika."
}