GET /api/v0.1/hansard/entries/1267973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1267973,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267973/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, ninachukua nafasi hii kusema asante kwa kunipa nafasi niongee kuhusu Mswada huu. Kwanza, ninampa kongole Sen. Mumma kwa kuleta Mswada huu hapa Bunge la Seneti. Mswada huu ni wa maana sana. Kama wenzangu walivyosema, tunaongea kuhusu maswala ya maendeleo katika dunia nzima. Mataifa ya dunia yalikubaliana kwamba kuna vipengele 17 ambavyo mataifa yote duniani yanafaa kuhakikisha vinafanyika katika nchi zao ili dunia nzima ipate maendeleo. Kenya ilijiandikisha kama moja ya mataifa ambayo yanadhamiria kufanya maendeleo na kupata vipengele 17 vifanyike katika nchi yetu. Mswada huu unalenga kuleta vipengele ambavyo vitahakikisha ya kwamba kuna ripoti ambayo inatoka Serikali kuu na nyingine kwa serikali za ugatuzi. Serikali za ugatuzi zinafaa kufuatilia mipangilio ya kuleta vipengele 17, kuhakikisha vinafanyiwa kazi namna gani katika gatuzi zao. Pia, Serikali kuu inafanya bidii gani kuhakikisha vipengele hivyo vinafanyiwa kazi, ama barabara gani inatumika ili wanainchi wa Kenya na dunia nzima iweze kuendelea mbele? Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu kipengele cha kwanza kinasema kwamba duniani kusiwe na njaa; no poverty . Ukiangalia saa hii, gatuzi zote za Kenya, ukiongeza gatuzi letu la Tana River, hakuna namna amabayo imewekwa katika sheria ambayo inamsukuma gavana wa kaunti kutoa habari kuhusu hali ya njaa. Kwa sasa, hakuna mechanism ambayo inamshurutisha Rais kutoa habari kuhusu kipengele cha kwanza cha vipengele 17 ambavyo vilikubalika katika dunia nzima, aelezee kuhusu mambo ya njaa katika nchi ya Kenya. Tukirudi katika kipengele hiki, kwa sasa zote tunafurahi hasa sisi ambao tunatoka katika gatuzi la Tana River na wengine ambao wanatoka sehemu ambazo tumepata mvua. Tunamshukuru Mungu kwamba mvua imekuja. Lakini, tunajua kwamba baada ya mvua, kutakuwa na kiangazi. Sasa mipangilio ya kuhakikisha ya kwamba wanainchi na mifugo haitapata shida, tukifuatilia hicho kipengele cha kwanza, hatujaona gavana akiongelea kuhusu hayo. Ndio maana tukipitisha Mswada huu, utashurutisha sio gavana wa Tana River tu, lakina magavana wote wawe wanapanga mipangilio ili wanainchi wasife njaa. Kipengele cha pili kinaongelea kuhusu kuondoa umaskini. Umaskini ni shida ni ya kibinafsi. Watu wetu wengi wanakosa pesa na namna ya kujikimu? Lakini, viongozi ambao tumewapa nafasi ya kuendelesha gatuzi zetu hauwasikii wakiongea ama kuzungumzia kuhusu umaskini katika gatuzi zao. Kwa mfano, hausikii magavana hao wakiongea kuhusu shida ya ukosefu ama uchochole katika Kaunti ya Nairobi. Ndio, kuna watu ambao wako sawa lakini kuna wengi ambao wanaumia. Hausikii Miswada kama hiyo ikiongelewa na magavana au kaunti zetu zote. Ndio maana, Mswada ambao Sen. Mumma ameuleta unatufaa sana kwa sababu utaleta mamna ya kupima. Kila wakati magavana wanapata nafasi, wanakuja kuongea kuhusu mambo ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}