GET /api/v0.1/hansard/entries/1267974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1267974,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267974/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "uchumi, ukosefu wa chakula na mambo ya elimu. Sio education tu lakini katika kipengele hiki wanasema quality education. Gatuzi letu la Tana River utakuta kuna sehemu ambazo shule ziko sawa. Lakini, ukiingia huko ndani, utakuta sehemu ambazo hakuna madawati na madarasa ya kutosha na wengine bado wanakaa chini ya miti katika gatuzi lilo hilo. Tukiongea kuhusu mambo ya quality education, wengine wanapata education ilhali wengine wanakosa kupata hiyo quality kwa sababu ya hali ambayo wanapanga mambo yao. Ikiwa Mswada huu utapita vile tunavyoomba, tunajua ya kwamba gatuzi zote zitawajibika na ziweze kusawazisha sehemu zote za elimu hapa Kenya. Kuna issue ambayo inaendelea hapa. Moja ya vile vipengele vya kuonyesha kuwa tunaendelea ni kuwa ma maji safi. Saa hii, mwenzangu ameongea kuhusu gatuzi la Nairobi. Lakini gatuzi la Tana River, sehemu nyingi sana watu wanalia, hakuna maji safi. Tena sisi tuna Mto Tana ambao hauishi maji. Ni mto ambao siku zote, kutoka Januari mpaka Desemba uko ma maji. Hata hivyo, Gavana wa Tana River na Tana River Water and Sewerage Company (TAWASCO), hawajapanga namna ya kuhakikisha ya kwamba watu wanapata maji ya kutosha ili kumaliza uchochole na magonjwa kwa wanainchi wa Tana River. Jambo la kushangaza ni ukienda upande wa Bura, Hola, ambayo ni jiji kuu la Tana River, na Garsen ambayo ni moja ya majiji makubwa, hakuna maji. Unapata watu wanakaa bila maji mwezi nzima. Watu wanakosa maji kisha ada ya maji inakuja kutoka Tana River Water and Sewerage Company (TAWASCO) ikiwahitaji walipe maji ilhali hakuna maji wamepata. Tunataka Mswada huu upitishwe na Seneta wote. Tuunge mkono ili sheria hii ikipita, Magavana wote; sio tu wale wa Kaunti ya Tana River; washurutishwe kutoa ripoti ya hali ya maendeleo ya maji. Watoto wetu wanapata magonjwa. Wengine wanapata shida na kusumbuka sana. Ukitazama picha jioni za miji yetu mikubwa katika gatuzi zetu unashangaa nini kinachoendelea."
}