GET /api/v0.1/hansard/entries/1267976/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1267976,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1267976/?format=api",
"text_counter": 191,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hoja hii ikipitishwa Magavana wataingia na shurutisho la kuwasaidia wananchi. Tunawaona magavana ambao wanamaliza mihula yao na kuna wengine wamehudumu mihula miwili. Nyumba na magari yao ni ya kifahari na maisha yao ni mazuri. Maisha ya uchochole ya wananchi ni yale yale. Tunataka vipengele hivi 17 visaidie wananchi na hata dunia nzima kwa sababu bado tunaona kuwa shida ni zile zile."
}