GET /api/v0.1/hansard/entries/1268002/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268002,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268002/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Okenyuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wananchi katika nchi hii wako na shida katika sekta ya kilimo, kupata umeme, afya ya uzazi na elimu. Pengine Sen. Mumma ambaye amewasilisha mwenye Hoja hii, amepata nafasi ya kutukumbusha kuwa sisi kama viongozi tunapotaka kuleta mabadiliko, haitachukua siku moja tu bali muda. Ndiposa NInapenda kuwakumbusha wale wenzetu wa upande wa upinzani kuwa Rais William Ruto ameonyesha ueledi na ameweka mikakati tofauti. Hivi karibuni, tutaona bei ya vyakula ikishuka. Kwa nini? Kwa sasa wakulima wengi wamepata mbolea ya bei nafuu na hatutaona watu wakienda kuandamana kwenye barabara kwa sababu chakula kitakuwa kwa wingi. Hii ni njia moja. Sehemu tofauti katika kaunti zinaweza kuleta miundombinu mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata vyakula na wao kama viongozi wajiunge pamoja nao. Hata kama uko kwenye sehemu ambayo haiko serikalini wakati huu, cha muhimu ni kuangalia wananchi waliokupigia kura. Ninaunga mkono Hoja hii mkono kwa sababu, vijana hawajajihusisha na kilimo. Pengine Hoja hii inatupa fursa ya kuangalia mambo ambayo kaunti zetu zinaweza kufanya ili kuwasaidia vijana kuwa na mipango tofauti kwenye sekta ya ukulima. Taifa hili linategemea ukulima kulisha wananchi na kufanya biashara. Pengine vijana wakiwekwa katika sekta hii ya kilimo, labda tutaona mabadiliko. Vijana wanafaa kufuata nyayo zilizoachwa na wale waliowatangulia. Nimefurahishwa na Hoja hii ya Sen. Mumma. Nimefurahi kwamba leo, umeona ni muhimu kutukumbusha sisi viongozi, kwamba kuna mambo ambayo tunafaa kufuatilia. Ili Ruwaza ya Mwaka 2030 isisalie ndoto tu, lazima sisi kama viongozi tutie bidii ili itendeke. Bw. Naibu Spika, leo nimejaribu kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili, nikifuata mkondo wa Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, ambaye alileta Kauli Bungeni. Sisi tunakienzi Kiswahili. Umoja wa Kimataifa umekipa Kiswahili nafasi ya kipekee. Mimi kama kijana mtungaji sheria, ninashabikia mkondo huo. Kama Wakenya pia, tunashabikia mkondo huo."
}