GET /api/v0.1/hansard/entries/1268244/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268244,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268244/?format=api",
    "text_counter": 201,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kuunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na ndugu yetu, Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi ndani ya Bunge hili. Kwa mara ya kwanza, nitakuwa mbunifu na kusema napiga support kubwa sana kwenye Bill hii kwa sababu imeweza kushika watu wengi sana. Kwanza, alisahau kutaja Gavana wangu wa Mombasa, Abdullswamad Shariff Nassir, aliyekuwa miongoni mwa magavana bora zaidi humu nchini. Aliongoza miongoni mwa magavana ambao wamekusanya ushuru. Ningependa kwanza kumpongeza Gavana wangu Abdullswamad. Mheshimiwa Spika wa Muda, imekuwa dhahiri shahiri kwamba kuna wale ambao wana mashamba na wamejenga nyumba lakini hawana chochote. Wamekuwa wakitoa ushuru sawia na wale ambao pengine wamejenga nyumba na kuweka wapangaji na wanakusanya mapeni. Kwa hivyo, nimeifurahia sana hii Bill ya leo kwa sababu yule mnyonge ambaye hana kitu atapata mwanya wa kutafuta wakati ambapo atakuwa sawa. Anaweza pia kufanya maendeleo na akalipa ushuru sawia na wenzake. Ningependa pia kumuunga mkono mwenzangu kwa hili; kuna watu ambao walikuwa wameajiriwa lakini sasa miaka imepita na wanafaa kustaafu na katika mashamba yao mijini wamejenga tu nyumba zao. Hawana mpangaji wala yeyote wa kuwasaidia isipokuwa pale ni makao yao. Watu kama hao wasiwekwe sawia na watu ambao wanalipa ushuru mkubwa ule wa kukusanya rent. Ikiwezekana, ningeomba kwamba watu ambao hawana chochote wasilipe kabisa mpaka wakati ambapo wataanza kudevelop yale mashamba yao ndio waweze kulipa ushuru. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}