GET /api/v0.1/hansard/entries/1268245/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268245,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268245/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Ningependa pia kumpongeza Kiongozi wa Walio Wengi kwa Mswada huu kwa sababu kuna wale ambao wametoka mataifa ya nje na wamekuja kuchukua mashamba hapa Kenya, wamejenga, wame-invest na kuweka biashara zao. Huwezi kulinganisha biashara zao na ya Mkenya ambaye biashara yake ni duni. Ushuru ambao unakusanywa usiwe sawia na yule Mkenya halisi. Ikiwezekana huyu wa Kenya atoe ushuru kidogo. Huyu ambaye amekuja kufanya biashara hapa Kenya, atoe ushuru wa juu kidogo. Hata sisi tukienda katika mataifa yao, hatusazwi kule. Tunatozwa ushuru kama yule mtu ambaye ametoka taifa lingine kuja ku-invest katika mataifa yao. Kama Kenya, ni muhimu pia tuige mfano huo na tuweze kuwatoza hawa ushuru zaidi. Juzi nimekuwa Ethiopia na kuna kitu ambacho nilikipata kule na nikatamani kiwe kwenye taifa letu. Kule Ethiopia, mashamba yao hayauzwi kwa watu wa nje. Tunasema kuwa wakuja ni watu ambao wametoka nje ya taifa. Shamba linabaki na kama ni Kenya, basi linabaki ni la Wakenya tu. Utapata watu ambao wametoka mataifa mengine wamekuja wamechukua mashamba yetu na Mkenya anabaki bila chochote. Kule Ethiopia, sheria inawaruhusu wageni kuchukua shamba kwa sababu ya kuwekeza kwa muda fulani. Baada ya muda fulani, wanaachia watu mashamba yao. Lakini hapa Kenya ni tofauti. Mtu ananunua shamba na ana-enjoy . Pengine alipata yule Mkenya halisi na matatizo kidogo na kwa sababu hajui thamani ya shamba lake, anaiuza kwa bei ya chini. Yule Mkenya anabaki anahangaika na watoto, na anakuwa maskini. Ningependa sheria ya Ethiopia kuhusu wawekezaji wageni ije hapa Kenya, lakini ni ya siku nyingine ambayo tutaweza kujadili hapa Bungeni. Kuna pia sintofahamu katika wale ambao wamechukua mashamba ndani ya miji. Pengine walipewa allotment notice, lakini ikawa kizungumkuti kupewa title deeds . Hili ni jambo ambalo ningependa pia Leader of the Majority Party aligusie ili mtu akipewa allotmentnotice baada ya kununua shamba, pengine kwa county government, basi ifuatane kabisa na ile"
}