GET /api/v0.1/hansard/entries/1268249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268249/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "pia ziangalie jambo hili; kuna mtu amekaa miaka mingi sana kwenye shamba na analipa ushuru. Pengine a merenew na analipa tena. Tuangalie pia watu hawa kwa jicho la upole ili hata kama wanalipa ushuru, basi wawe na furaha ya kuweza kulipa. Masuala ya ushuru yamekuwa donda sugu na yenye utata katika taifa hili. Ningependa kumkosoa kidogo Leader of the Majority Party kwa kusema kuwa sisi tulikuwa barabarani. Ninataka kumuelewesha kuwa hatukuwa barabarani kwa kupenda; hali ya maisha imekuwa ngumu na tata. Hata yeye kesho ana nafasi ya kuingia kule barabarani ajieleze na akasikizwe. Katika jambo hili la mashamba, ninampongeza sana. Hili litaleta uchumi bora katika taifa letu. Kwa wale ambao wana mashamba na pengine nyumba ambazo wamepangisha, nawaomba msiwe mnachelewesha ushuru kwa sababu unatumiwa kujenga taifa. Ushuru ukikawia sana, mambo yanaenda mrama. Unapata kuwa yule Mkenya wa tabaka la chini kabisa anahangaika. Tujibidiishe sana kulipa ushuru na tuangalie kuwa ushuru ukitolewa, basi pesa zikikusanywa ziende kwa mifuko ambayo italeta tajriba katika jamii. Ushuru uende kwenye mifuko ambayo italeta maendeleo katika jamii. Mhe. Spika wa Muda, pesa hizo ziende kwenye mfuko wa kuonyesha kuwa Wakenya wametoa ushuru lakini kuna maendeleo yanayoonekana. Wale ambao ni wanyonge katika jamii pia nao waangaliwe katika mifuko yao. Hii yote inatokana na kulipa ushuru kwa wakati. Nikiendelea kuunga mkono mjadala huu, ningependa kusema kuwa kule Mombasa County kuna ndugu zetu ambao walikaa kule miaka mingi sana na hawajapata hati miliki za mashamba yao lakini kuna watu ambao wanachukua ushuru wa mashamba yale ilhali wao si wakaazi wa Mombasa. Nimeitwa na wazee ambao ni Council of Elders wa Mombasa na wakanilalamikia sana kuhusu jambo hili. Unapata kuwa mwananchi wa Taifa la Oman ndiye anayekusanya ushuru kutoka kwa yale majumba Mombasa County. Naiomba County Government ya Mombasa ifuatilie jambo hili na mimi kama mama County wa Mombasa niweze pia kulileta suala hili bungeni ili tuweze The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}