GET /api/v0.1/hansard/entries/1268251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268251,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268251/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, mjadala huu wa leo ni mpana sana. Nawapongeza wenzangu na kutilia pondo ujuzi ambao umejitokeza leo kwa kusema kuwa wawekezaji kutoka nje wasilipe ushuru sawia na Wakenya ila walipe ushuru wa juu kidogo. Hiyo ndio sheria ambayo tunataka. Isiwe kuwa Wakenya wananyanyaswa. Mtu akipata pesa kidogo anawaza iwapo atalipa ushuru ama atanunua chakula. Wakenya waliokaa miaka mingi katika hayo mashamba wapunguziwe ushuru kwa sababu hali ya maisha ni tata sana. Wale waliokuja ku-invest kwenye sekta ya ujenzi wa nyumba za magorofa wanakusanya kiasi kikubwa cha rent na hivyo basi wanapaswa kulipa ushuru kwa wakati unaofaa."
}