GET /api/v0.1/hansard/entries/1268517/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268517,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268517/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, nimesimama kuambatana na Kifungu cha 52 (1), cha Kanuni za Kudumu za Seneti kutoa Kauli kuhusu siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili iliyoadhimishwa mnamo Tarehe 7 Julai, 2023. Bw. Spika, Kiswahili ni Lugha ambayo inatumiwa na kuzungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 katika Bara la Afrika. Hii ndiyo lugha inayokuwa na kusambaa kwa kasi zaidi ulimwenguni, ikizingatiwa kuwa mataifa ya Uchina na Japan yameanza kufunza lugha hii nchini mwao. Afrika Kusini pia ni taifa ambalo lugha hii imeanza kufunzwa. Moja ya maazimio ya Umoja wa Afrika ni kwamba siku moja lugha yetu hii ndiyo itakayo kuwa lugha rasmi ya Bara la Afrika. Bw. Spika, Mwaka huu wa 2023 maadhimisho rasmi ya siku ya Kiswahili duniani yalifanyika Jijini Kampala, Uganda, na yaliongozwa na Baraza la Lugha ya Kiswahili la Afrika Mashariki; kwa kiingereza, East Africa Swahili Council. Ni Jambo la kutia moyo kuwa nchi ya Uganda imekubali kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi nchini humo. Habari kama hizi ni zakutia moyo ikitambulika kwamba Kiswahili ni lugha inayotumika Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Mashariki mwa Congo (DRC) kwa wingi. Mataifa yote haya ni Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}