GET /api/v0.1/hansard/entries/1268518/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268518,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268518/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Nchini Kenya, sherehe hizi ziliadhimishwa na jamii ya Waswahili katika eneo la Mama Ngina Water Front, Kaunti ya Mombasa. Maeneo haya ni baadhi ya turathi za Waswahili na mahali hapa tangu zamani palijulikana kama Mzimle. Bw. Spika, wakati maadhimisho haya yakifanyika, inapaswa tuzingatie hatua tulizopiga katika kuendeleza lugha ya Kiswahili. Hapa Seneti tumeweza kufasiri Kanuni zetu za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili lakini bado zipo hatua nyingi zinazofaa kupigwa ili tuwe na matumizi ya Kiswahili katika Seneti. Kwa mfano, bado hatuweza kufasiri Miswada ya Sheria, Ardhihali na ripoti za kamati kwa lugha ya Kiswahili. Hatua hii itasaidia pakubwa kuwapa ufahamu Wananchi ambao wanafuatilia maswala Bungeni. Natumai tutafikia hatua ya kuwa na Miswada ya Sheria iliyo chapishwa kwa lugha ya Kiswahili kabla ya mwisho wa muhula wa Bunge hili. Bw. Spika, katika nyanja nyingine hatua pia zimepigwa kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili. Hivi Majuzi Mahakama Kuu hapa Nairobi, ilisikiliza kesi ya kwanza iliyo wasilishwa kwa lugha ya Kiswahili na Wakili Kinyanjui. Wakili huyu alisisitiza kuendesha kesi yake kwa lugha ya Kiswahili jambo lililompa mshangao Wakili wa upande wa Utetezi. Hii ni hatua kubwa kwa sababu wananchi wengi wanapokuwa Mahakamani hawaelewi kesi zao zinavyoendeshwa na hivyo basi kusababisha wao kukosa Mahakamani. Lugha ni kati ya mambo ya tamaduni ambazo zinatambuliwa Kikatiba. Lakini ukiangalia bajeti zinazo tengwa kwa huduma hii, utapata kwamba ni haba sana kiasi ambacho Kaunti zetu hazina chochote ambacho wanaweza kujivunia katika nyanja hii. Naona ipo haja kutenga rasilmali za kutosha ili kuimarisha maswala ya kiasli na tamaduni zetu katika Kaunti zetu. Jamii na hasa wazee wa jamii ya Waswahili wanaitaka Serikali ya Kitaifa iwarudishie Mama Ngina Waterfront iliyo Jijini Mombasa ambalo ni turathi ya Waswahili ili waipe turathi hiyo jina lake asili ambalo ni Mzimle. Bw. Spika, wakati tunapigania kurejeshwa kwa turathi zetu kutoka kwa Wakolini, ni aibu kwamba hapa nchini Kenya zile turathi ambazo zimechukuliwa na Serikali ya Kitaifa hazijawezwa kuregeshwa katika Kaunti zetu. Ningependa kumaliza kwa kutoa rambirambi zangu na za Watu wa Mombasa kwa kumpoteza Prof. Mohamed Abdulaziz ambaye alikuwa Mkufunzi wa Lugha Chuo Kikuu cha Nairobi katika kitengo cha Kiswahili. Almarhum Prof. Abdulaziz ametoa mchango mkubwa katika kufunza Lugha ya Kiswahili na ameacha pengo kubwa hususan kwetu sisi Waswahili Kindakindaki. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pema peponi. Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii."
}