GET /api/v0.1/hansard/entries/1268524/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268524,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268524/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, nimesimama chini ya kifungu cha 52(1) cha Kanuni za Kudumu za Seneti kutoa Kauli kuhusu swala la kitaifa kuhusiana na kuzorota huduma za feri katika kivuko cha Likoni. Mheshimiwa Spika, kivuko cha Likoni kinaunganisha sehemu ya Pwani kusini na kisiwa cha Mombasa. Vile vile, kinaunganisha Kenya na Tanzania kupitia barabara ya Malindi-LungaLunga-Horohoro-Tanga-Bagamoyo. Barabara hii ni ya kimataifa. Kina umuhimu mkubwa kwa maisha ya wanabiashara, sio kwa kaunti za Mombasa na Kwale pekee, bali pia kwa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Hivi karibuni, huduma katika kivuko hicho zimedorora sana. Kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari na watu wanaotumia kivuko hicho. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni, kulitokea mkasa ambapo bibi mmoja na binti yake walipoteza maisha yao wakati gari lao lilipo tumbukia baharini wakiwa ndani ya ferry, iliyowachukua kutoka Likoni Kusini kuja katika kisiwani cha Mombasa. Mheshimiwa Spika, hadi leo hatujui ni nani anapaswa kuwajibika kwa ajali hiyo. Mnamo mwaka wa 1993, ferry la mtongwe lilizama na zaidi ya watu 250 wakapoteza maisha yao. Hadi leo, bado kuna familia zinazosubiri fidia ya wapendwa wao. Mikasa yote hii inaashiria umuhimu wa usalama wa binadamu na mali izingatiwe katika kivuko hicho. Wiki mbili zilizopita, Halmashauri ya Bandari inayosimamia ferry za kivuko hicho, lilifunga daraja ya miguu linalotumiwa na wananchi wengi kuvuka kutoka Likoni kuingia mjini Mombasa. Hii imesababisha msongamano mkubwa katika kivuko hicho cha Likoni. Vile vile, huduma za ferry ya Mtongwe zilizoondolewa, hivyo kuwabidi watu wengi kutumia ferry ya Likoni ili kuenda kisiwani kwa biashara na ajira. Mheshimiwa Spika, kuna ferry nne ambazo zinazohudumu lakini, mbili peke yake ndizo ambazo zilinunuliwa hivi karibuni. Zingine ni za zamani sana na haziwezi kuhudumu masaa yote bila kupumzishwa. Kutokana na ongezeko la watu katika maeneo ya Likoni, ni muhimu ferry hizi ziweze kuwa katika hali nzuri ili wananchi wasitatizike wakati wanatumia kivuko hicho. Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Bandari, Nahodha William Kipkemboi Ruto, alinukuliwa akisema kwamba ukarabati wa daraja la kuvukia kwa miguu kutoka Likoni hadi kisiwani cha Mombasa utachukua miezi kadhaa kukamilika. Mkurugenzi huyo pia alizindua huduma za kuingiza meli kwa masaa ishirini na nne katika bandari ya Mombasa. Hivyo basi, ina maana kwamba meli zitaweza kutia nanga katika bandari hiyo wakati wowote, kinyume na hapo awali ambapo zilizuiliwa wakati wa asubuhi mapema na alasiri kwa sababu daraja la wanaopita kwa miguu huwa limefunguliwa. Kauli hizi mbili za Mkurugenzi huyo, zimeleta utata kwa sababu iwapo meli zitaingia bandarini masaa ishirini na manne, daraja la wanaopita kwa miguu halitafunguliwa tena. Hii itasababisha msongamano kuendelea katika kivuko cha ferry cha Likoni. Nikiongezea, hatujapokea ripoti za mipango ya ununuzi wa ferry nyingine katika miaka ya hivi karibuni, hatua ambayo ingesaidia kutatua msongamano wa wananchi katika kivuko hicho. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}