GET /api/v0.1/hansard/entries/1268525/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268525,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268525/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Mheshimiwa Spika, hili daraja la miguu lilianzishwa 2020 na liligharimu Serikali karibu Kshs1.4 bilioni. Daraja ni jipya na halina sababu ya kurekebishwa kwa muda mrefu kama vile ilivyopangwa. Itakumbukwa kwamba, daraja la kuvukia kwa miguu kwa wasafiri wanaotembea kutoka Likoni hadi kisiwani lilizinduliwa wakati wa janga la Corona, ili kuondoa msongamano na kurahisisha usafiri. Kwa hivyo, kabla ya kulifunga daraja hili, ni muhimu kwa Halmashauri ya Bandari kuweka mikakati mbadala kupunguza msongamano katika kivuko cha Likoni. Kuna wawekezaji wanaomiliki vyombo vya usafiri baharini na ambao wako tayari kutoa huduma hizo katika kivuko cha Likoni, lakini Halmashauri ya Bandari imekataa kuwapa kibali cha kutoa huduma hizo. Swala hili lina umuhimu mkubwa sana na naomba Kamati husika kulivalia njuga swala hili, wazuru eneo hili ili wajionee masaibu wanayopata wananchi wa Likoni na wale wanaokwenda nchi jirani ya Tanzania. Asante, Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa hii."
}