GET /api/v0.1/hansard/entries/1268554/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268554,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268554/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niseme maoni yangu kuhusu Mswada wa Kiswahili ulioletwa na Sen. Faki. Katika mkutano wa 41 wa United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) tarehe 23 Novemba, ilipitishwa ya kwamba Kiswahili kiwe kinatumika katika mikutano ya kimataifa. Zaidi ni kwamba siku ya Kiswahili ilipitishwa kuwa tarehe saba Julai kila mwaka. Kiswahili kilikuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambulika na kupitishwa katika Baraza hilo la Umoja wa Mataifa. Bw. Spika, kama alivyosema Sen. Faki, tarehe saba Julai ilitawazwa hapa Kenya na Uganda. Hata hivyo, kisichotosha wala hakistahili ni kwamba hatujaona sherehe za kustahi Kiswahili katika kaunti zetu na Serikali Kuu. Tungependa sana Kenya ikuwe mbele kati ya yale mataifa ambayo yanastahi Kiswahili. Kwa hivyo, ningependa kuchukua nafasi hii kuuliza Serikali Kuu na za kaunti, zipangie vizuri sherehe za siku ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili tarehe saba Julai mwaka ujao. Bw. Spika, katika Bunge la Afrika, wakati mwingine tunasimama na kuzungumza Kiswahili. Kusema kweli, watu wengi hufurahia kwa sababu Kiswahili ni lugha pekee ya Kiafrika ambayo inatambulika katika Pan-African Parliament (PAP). Tunaomba Kenya iwe mstari wa mbele kupatia lugha ya Kiswahili heshima kama jinsi ilivyoheshimika katika nyanda za Afrika na kote duniani."
}