GET /api/v0.1/hansard/entries/1268565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268565/?format=api",
"text_counter": 210,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "sababu sisi viongozi wa pwani tuko mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Serikali yetu ya Kenya Kwanza inatufungulia anga ili utalii uweze kuboreka. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba mtalii anafika Mombasa na akwame pale feri kwa sababu ya msongamano. Hivi majuzi tu katika likizo yetu fupi, mimi mwenyewe nimekwama pale takriban masaa manne. Katika hali ile, nilitangamana na wafanyikazi wa feri na wakanieleza shida yao kubwa zaidi ni nyongeza ya mshahara. Tumepoteza wawekezaji, biashara na ajira kwa vijana wetu kwa sababu ya msongamano huu. Ninaomba Kamati husika ilivalie njuga swala hili. Isikize vizuri na ifanye uchunguzi wao kwa kina ili tuhakikishe huduma za feri zimeboreshwa. Vile vile, ninampongeza Sen. Faki kwa ile kauli yake ya Kiswahili. Kiswahili ni lugha ya taifa. Kiswahili kinaleta uwiano na utangamano dunia nzima. Kwa hivyo, ni ombi langu kwamba sisi kama viongozi katika Bunge hili, tuichukue kauli ya Sen. Faki kwa kikamilifu zaidi na tutukuze Kiswahili."
}