GET /api/v0.1/hansard/entries/1268654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268654,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268654/?format=api",
"text_counter": 299,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii na mimi nizungumzie Mswada huu. Kwanza kabisa, ninamshukuru Sen. Mariam Omar kwa kuleta Mswada huu unaohusu usawazishaji wa leseni na njia za kutoa leseni katika magatuzi yote 47. Ninampongeza Seneta kwa sababu kazi yake inaonekana kila wakati akileta Miswada yake hapa. Tunampa motisha aendelee na kazi hii. Bw. Spika wa Muda, leseni ni muhimu kwa sababu zinampa mtu nafasi ya kufanya biashara bila wasiwasi. Inampa mfanyibiashara yeyote nafasi ya kufanya kazi yake akijua katika vitabu vya Serikali – ya gatuzi ama Serikali kuu – jina na biashara zake zinajulikana kirasmi na anapofanya ile kazi hana wasiwasi. Sisi kutoka Kaunti ya Tana River ni wakuzaji wa maembe, tikiti maji, pojo na maharagwe. Sisi pia ni wafugaji. Mara nyingi gatuzi letu linatoa mbuzi, ng’ombe na ngamia kwa masoko yetu. Wengi wa wanabiashara wanaokuja kununua wanatoka nje. Wakija, wanakuja na leseni zao kuchukua hii mali kwenda kutafuta soko. Shida yetu ni kwamba wanabiashara ambao wanakuja kwa gatuzi letu wanasumbuliwa na kutesaka sana. Sisi wenyewe, kama unasafirisha maembe yako kutoka Tana River kwenda kuyauza katika Kaunti ya Kilifi au Mombasa kupitia barabara, sisi pia tunasumbuliwa sana barabarani. Hata kama umekata leseni yako, tunapata shida. Hii ni kwa sababu hakuna usawazishaji wa hizi leseni. Sheria hii mpya ambayo imekuja italeta hali ya kupumua kwa wafanyibiashara. Hii ni kwa sababu sasa mfanyibiashara akitoka na miraa yake huko Meru, apite Tharaka- Nithi mpaka Tana River anakonuia kuuza, basi safari yake itakuwa nzuri na ya kupendeza zaidi. Ni bora hivyo kuliko kama mambo ya hii leseni yanasumbua vilivyo kwa sasa. Bw. Spika wa Muda, tunataka Bunge la Seneti lipitishe sheria hii kwa haraka sana. Tunaomba kila Seneta ambaye atasimama apitishe hii sheria kwa haraka sana. Ninasema hivi kwa sababu itakuwa rahisi kwa mfanyibiashara kusafirisha bidhaa hadi sokoni na ile leseni aliyokata kwa kuwa inajulikana na askari wa kaunti na Serikali Kuu. Kwa sasa, ipo shida na wenzangu wameshazungumzia shida ambazo watu wa biashara wanapata. Sisi kule chini sehemu kama Hewani, Kulesa na Wema, watu wakishatoa matunda shambani, unakuta wafanyibiashara wanakuja pale na wanasema lazima washushe bei ya kununua kwa sababu wamepata shida huko njiani. Kwa mfano, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}