GET /api/v0.1/hansard/entries/1268655/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268655,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268655/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "pengine wameweka lori ya kwanza, walinunua kwa pesa fulani lakini mara ya pili, wanaanza kulia bei kwa sababu wamesumbuliwa sana barabarani kuhusu leseni. Wale wanaofanya kazi sokoni ya mifugo pale sokoni, Garsen ama kule juu sehemu za Bangali, wanapata shida sana. Hii ni kwa sababu, kati ya wale wanabiashara ambao wanakuja kunua, wanasema bei lazima ishike kwa sababu ya kusumbuliwa barabarani kuhusu leseni. Hii ndio maana leo ninasimama hapa kusema tuipitishe hii sheria ya kusawazisha taratibu zote za kukata hizi leseni. Kifungu cha Saba katika hii sheria kinasema kwamba kila gatuzi na kila mamlaka ya kukata leseni inatakikana baada ya hii sheria kupitishwa, miaka mitatu isipite kabla wao hawajaweka hii system yote kwa kompyuta. Mambo ya ufisadi yataisha. Ikiwa mtu atafuata zile taratibu na kukata leseni yake, akija Tana River kununua mifugo au vyakula, akisimamishwa na polisi, ataonyesha tu leseni na amweleze polisi kwamba ashalipia kila kitu wala asisumbuliwe tena na mambo ya pesa. Ukienda nchi kama Afrika Kusini, hata saa zile unaingia katika lango kuu, sioni mtu akija na kikaratasi pale ama kitabu aandike kuwa wewe jina lako ni nani na leseni yako ni namba ngapi. Mtu anakuja na kitu cha kompyuta na kukiweka karibu na karatasi yako. Kama ni leseni, inaonyesha automatically kwamba leseni yako iko sawa, wala hupotezi wakati. Wakati mwingine, hizo leseni zimebandikwa katika kioo cha gari. Sasa mtu anapofika pale, askari au kanjo anaweka ile mashine ya compyuta na hilo gari linapita bila kupoteza wakati. Bw. Spika wa Muda, sisi tunataka Kenya pia iendelee. Tunataka wanabiashara wetu waendelee. Ikiwa mtu amekata leseni na anapeleka miraa yake Tana River ama kokote kule, haina haja kupoteza wakati. Haina haja polisi kuwashika watu na kuchukua hongo. Muhimu ni kuweka ile leseni kwa gari ama dereva akuwe nayo ili mtu akipita, kifaa cha kompyuta kinasoma na mtu anapita. Kama umebeba mifugo unapita. Hakuna mambo ya kusumbuliwa na kuulizwa karatasi hii au ile, mara polisi anakuita nyuma ya gari au kona fulani akikuambia uongeze maanake hii haitoshi. Huku ni kupotezeana wakati na pesa zinapotea namna hii, huku ufisadi ukizidi kuongezeka kwa sababu ya kukosa sheria ya kusimamia mambo haya. Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, nimefurahi sana jinsi hii sheria ilivyotungwa. Hata hivyo, kuna kipengele ambacho ninaona kimekosekana. Naomba Sen. Mariam Omar aangalie kifungu hicho kwa sababu ufisadi ni jambo kubwa sana. Naomba aangalie jinsi sheria zinavyotungwa kule Afrika Kusini na nchi zingine za Marekani na Ulaya. Ni nini ambacho kitafanywa ili wanabiashara ambao wanazingatia sheria zote waweze kufanya kazi bila kusumbuliwa na askari wa magatuzi? Kuna pengo pia katika Kifungu cha Saba. Hakupeana adhabu kwa licensing"
}