GET /api/v0.1/hansard/entries/1268836/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268836,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268836/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": " Nakushukuru Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Pia, ninamshukuru Mjumbe wa Kirinyaga, Bi. Jane Maina, kwa kuleta Hoja hii mbele ya Bunge hili. Langu litakuwa tu onyo kidogo. Kama tunavyosema tumeiweka wazi na kusema ni comprehensive, au kwa upana, tunataka kuwe na hii elimu ya kujamiiana katika shule, lazima tuwe na tahadhari. Kwa sababu, tukiiweka kwa upana zaidi kuliko vile ilivyo, huenda kukatokea mambo ambayo yataingizwa ndani yake na kudhuru vijana wetu. Tunaujua mtaala mzima wa jambo hili la elimu ya kujamiiana kwa Kiswahili. Ni jambo ambalo linaweza kuleta madhara makuu, na itakuwa sivyo tulivyokuwa tumeelekeza kidole chetu. Inaweza kuleta madhara na ikatudhuru sisi. Mimi kama Mjumbe kutoka sehemu ya Kwale, ninasema kuwe na utaratibu maalum wa kukinga na kupenyeza maneno ambayo hatukuwa tumeyatarajia. Tunajua kwa kweli watoto wetu wanahitaji hii elimu na kufunzwa ni jinsi gani miili yao imegeuka, na kupokea hisia zingine tofauti zinazoonyesha kuwa wao wamekuwa watu wazima. Wao pia hupenda kuonja au kujaribu kila kitu wanachokisikia na wanachokiona. Tunajua mitandao imefungua njia zote. Watoto wanajua mambo mengi yaliyo katika ulimwengu kushinda hata sisi wazazi."
}