GET /api/v0.1/hansard/entries/1268844/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268844,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268844/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. dadangu Jane kwa kunifahamisha hivyo. Yangu tu ilikuwa ni kutilia mkazo. Tunajua kuna utaalam mwingi na hususan Wajumbe wale wanaojua sana maswala ya sheria. Mara nyingine muwe mkifafanua zaidi kwetu sisi ili tuelewe zaidi. Kwa hivyo ninasema asante. Nilikuwa nimefikia pale kwa kusema, sehemu kama ile ninayotoka ya Kwale, vijana wengi wameathirika na swala hili la kujamiiana au sex education, kwa lugha ya Kimombo. Hii ni kwa sababu tumetoka sehemu ya mashambani. Vijana hawana ujuzi wa mambo mengi sana, na wanapenda sana kujaribu jaribu kila kitu kile wanaona. Wakipata zile simu za rununu na kuziangalia, wanaona mambo ambayo ni ya kusisimua na kuvutia. Inamfanya aseme ‘wacha pia mimi nijaribu’. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}