GET /api/v0.1/hansard/entries/1268871/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1268871,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268871/?format=api",
    "text_counter": 198,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "kwa kutojua na wakajipata wameingia katika masuala machafu. Kuna wazazi wengine ambao nilikuwa nikizungumza nao na wakasema kuwa maisha yamekuwa sawa kwa sababu kuna teknolojia. Ingawa kuna teknolojia, lazima wazazi waweke mipaka kwa watoto wao ili wajue wanafika wapi. Mpe mtoto wako elimu na muda wa kusoma. Simu ikae kando. Kama anataka communication, afadhali umpigie mwalimu kisha uongee na mwana wako. Usimpatie mtoto simu ya rununu. Shetani amefichwa katika hizi simu. Nilipokuwa kule Mombasa, nilisitikika sana. Niliitwa na mwalimu mkuu wa shule moja na akaniambia kuwa shule yake imeharibika. Watoto wa kike wanajamiiana wenyewe kwa wenyewe. Ni jambo la kusikitisha. Kama sisi ni viongozi tunaotunga sheria katika Jumba hili, basi tuhakikishe tumeweka sheria ambayo haitavuka maadili ya dini na utamaduni wetu. Tuweke sheria ambazo zinaambatana na hali halisi ya mtoto wa Kiafrika na dini zetu."
}