GET /api/v0.1/hansard/entries/1268872/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1268872,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1268872/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Ninajua Mheshimiwa amegusia mambo mengi sana. Ninakumbuka tukiwa shuleni tulikuwa tunasomeshwa elimu ya ngono. Sijui kama kuna mahali ambapo walimu wamezembea kidogo na hawaelezei mambo haya kwa upana. Ninakumbuka nikiwa shuleni, mwalimu wetu alikuwa anatuita na kutufunza wazi wazi. Anachora ule mchoro wa viungo vya uzazi na kutueleza kuwa tukifanya hili na lile tunapofika hatua ya kuvunja ungo, mambo yatatuharibikia. Tulikuwa tunafunzwa kwa uwazi. Sijui ni kitu gani kilichopotea hapo katikati hadi sasa tunatunga sheria ya kuweka elimu ya ngono katika mtaala ilhali tayari iko katika elimu ya reproduction shuleni. Ndio maana nimekuwa na wasi wasi. Wakati Mhe. Jane alisema kuwa mambo mengine tofauti hayataongezwa, nilipata nafuu kidogo. Tunafanya mambo hapa kisha mtu mwingine aje kutoka kando na kusema kuwa ana haki ya kufanya ngono na mke mwenzake, ama mwanamume na mwanamume mwenzake, ama watoto waanze kufunzwa mambo tofauti shuleni. Hatutakubali hayo. Tutarudisha mjadala katika Jumba hili ili tupinge mambo kama hayo. Kwa leo, ninakupongeza sana mdogo wangu. Nina imani kuwa mambo haya yatafunzwa kwa upana kwa watoto wetu. Ninawahimiza ndugu zetu ambao ni wachungaji, maimamu na walimu wa madrasa wawafunze watoto wetu ili waweze kuelewa. Katika Uislamu, tunaambiwa kuwa la taqrabu zina. Usikurubie mambo ya ngono kabisa. Hawajatuambia tusifanye ngono. Wametuambia tusikurubie mambo ya ngono kabla ya kuolewa. Ndio maana mimi naringa leo. Niliolewa nikiwa bado fresh . Tufunze watoto wetu wasianze kuonjaonja “matunda”. Wakiolewa, “tunda” lao liwe liko safi ili wanapoingia katika ndoa, wanapewa heshima yao."
}