GET /api/v0.1/hansard/entries/1269172/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1269172,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1269172/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Ningependa kuchangia machache kuhusu Mswada ambao Seneta ameibua kwamba lazima serikali za kaunti ziwe na mfumo wa elektroniki utakao tumika kuhakikisha kwamba watu wanapata leseni zao kwa wakati unaostahili. Vile vile, kupitia mfumo huu, itakuwa rahisi kufuatilia ni watu wangapi wamesajiliwa na kupewa leseni za kufanya kazi katika kaunti husika. Mswada ambao Seneta ameleta, ni kuhakikisha kwamba Serikali itakuwa na kumbukumbu za majina, kampuni na biashara zinazohusika katika kaunti husika. Wakati ambao wanawasilisha stakabadhi zao kuhakikisha kwamba biashara zao zinapewa leseni ni rahisi serikali kupata stakabadhi, majina ya wenye kampuni na kampuni hizo zinafanya biashara zipi katika kaunti hizo. Bw. Spika wa Muda, kingine kinachodhihirika katika Mswada huo ni kuhakikisha kwamba wale ambao wamepewa leseni ama wamewasilisha stakabadhi zao, kupata leseni, ni lazima serikali kuwapa majibu kwa muda unaostahili. Itakapofika siku 28 kabla wao kupewa majibu, itakuwa kana kwamba serikali kwamba waendelee na kazi na kufanya biashara. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}