GET /api/v0.1/hansard/entries/1269173/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1269173,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1269173/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Sasa ni jukumu la serikali husika kupitia stakabadhi hizi na kuwapa walioomba nafasi majibu kwa wakati unaostahili. Wasipofanya hivyo, wanabiashara hao wataendelea kufanya kazi zao, kwa sababu, Mswada ulioletwa hapa unajukumisha washika dau katika kaunti kufanya kazi zao jinsi inavyostahili. Mhe. Spika wa Muda, mwisho kabisa, vijana na wale ambao ni chipukizi katika biashara wataweza kupata nafasi ya kulipia ushuru au leseni zao kwa awamu moja. Katika mfumo wa elektroniki, anapobonyeza na iwapo anataka kupata leseni mbali mbali, mfumo huu unamwezesha kupata idhini kwa wakati unaostahili na wakati huo. Sio jinsi inavyotendeka sasa. Wafanya biashara hao au wawekezeji hao wanatundika guu zao begani kutoka ofisi moja hadi nyingine kutafuta leseni. Mswada huu utafupisha gharama ya kazi, uekezaji na hivyo, kazi ifanyike jinsi inavyostahili. Kutoka kwangu, naunga mkono Mswada huu kuhakikisha kwamba nchi inasonga mbele."
}