GET /api/v0.1/hansard/entries/1269653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1269653,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1269653/?format=api",
    "text_counter": 368,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": " Shukrani, Mhe. Spika wa Muda. Kama Mbunge wa Laikipia Kaskazini, ninapenda kumshukuru Mhe. Rozaah na pia kumpa pole zangu, pole za akina mama wote na wazazi ambao wamepoteza watoto. Ninapenda kuongea kama mama. Waswahili husema mkuki kwa nguruwe ni mtamu na ni mchungu kwa binadamu. Lengo la Mhe. Rozaah kuwasilisha Hoja hii ni ili tujadiliane na tupate njia kabambe ya kuweza kutatua shida iliyo mbele yetu. Tuseme ukweli. Unajua uhuni haukubaliki iwapo unatoka kwa polisi ama raia. Kila mara tunakashifu polisi na tunasahau kwamba hawajatolewa nje ya nchi hii. Ni sisi tuliwazaa. Kuna shida kubwa sana Kenya tunapozungumza sasa hivi. Watu wengi wamesongwa na mawazo. Kumekuwa na matatizo ya akili na polisi hawajasazwa. Pia wao wako na hiyo shida. Ninaomba wakati tunapoongea maneno kama haya tuelewe kwamba kuna wazazi wanalia kwa sababu wamepoteza watoto. Kwa hivyo, tusiweke msumari moto kwenye kidonda. Lakini pia ndugu zetu kutoka upande wa upinzani, ningependa kuomba kwa heshima. Iwapo hawa vijana watakuwa wanakufa kila wiki, jameni na nyinyi teremsheni kiburi chenu na msimamishe haya maandamano. Iwapo hiyo haiwezekani, hakikisheni kwamba mara nyingine tukijadiliana hapa, Wabunge watatu wawe wamepigwa risasi ili tujue vile nyinyi mtasikia."
}