GET /api/v0.1/hansard/entries/1269656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1269656,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1269656/?format=api",
"text_counter": 371,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia North, JP",
"speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "moja nilipewa kichapo cha mbwa na polisi. Kwa hivyo, inastahili sisi kama Wabunge na Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa tuchunguze ili tujue haswa polisi na waandamanaji walifanya makosa gani. Tusianze kuzungumza kufurahisha nafsi zetu na kusahau kwamba iwapo Kenya itachomeka hamna nchi ingine mtaita nchi. Kenya ikichomeka, Kenya kwanza na Azimio zitachomeka. Mhe. Spika wa Muda, ningetaka kuwarai ndugu zetu. Tuliweza kuweka mfano mzuri wa kuigwa katika kanda ya Afrika na dunia nzima wakati tulipopiga kura. Ijapokuwa kiongozi wa Azimio hakukubaliana na uamuzi wa majaji, aliyaheshimu. Unajua kuna kukubaliana na kuheshimu. Hakukubaliana na uamuzi huo lakini aliuheshimu. Tuliweka mfano wa kuigwa katika dunia hii. Kwa hivyo, ndugu zangu, Waswahili wanasema mgema akisifiwa, tembo hulitia maji. Tusije tena tumeheshimika na punde si punde tuharibu hiyo heshima. Ndugu zangu, ninawaomba, mnapojadili Hoja hii, mfanye hivyo mkijua kwamba wale vijana ambao wamekufa ni watoto wa binadamu. Pia, polisi wamekufa. Na kama polisi walikufa, waliuawa na nani? Sidhani polisi waliuawa na polisi wenzao. Kuna makosa yametokea."
}