GET /api/v0.1/hansard/entries/1269959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1269959,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1269959/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Bw. Spika. Kwanza, ninawapa kongole walimu walioleta Taarifa hii. Tunaelewa ya kwamba sisi zote ni watu waliohitimu kutoka kwa akili na mafunzo ya walimu. Taarifa hii ni muhimu sana ndani ya Bunge hili la Seneti. Ya kwamba tuweze kuangalia matatizo yanayowakumba walimu katika sehemu zao zote wanazofanya kazi katika inchi nzima ya Kenya. Taarifa hii imeletwa na watu wa Kilifi. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Kilifi, ninajua matatizo yanayowakumba waalimu katika maeneo waliyoyataja hapa. Ninaona Petition hii ni ya haki na ukweli. Kuna sehemu zingine ndani ya Kaunti ya Kilifi ambazo zimefika katika kiwango ambacho mapato yao hayalingani na zile sehemu ambazo wanaketi. Ni sehemu ambazo hivi sasa ziko ghali na maisha pia iko ghali. Ndio sababu mimi ninasupport hii Petition . Ndugu zangu Maseneta, hili ni jambo muhimu ambalo linahusika na walimu. Sisi zote lazima tuungane pamoja ili tuunge mkono Petition hii."
}